140. Tumsifu sisi Watu
1. Tumsifu sisi watu, tumsifu Mungu Baba, aliyeumba vyote kwa nguvu yake kuu. Wazima watu wote, na ndege wa angani wanyama wa mwituni, kwa huruma yake. 2. Tumsifu sisi watu, tumsifu Bwana Yesu, aliyetukomboa kwa damu yake tu. Amani tumepewa, hatuna hofu tena Ametuhurumia, Mwokozi ni yeye. 3. Tumsifu sisi watu, tumsifu Roho, ndiye Mtulizaji popote, furaha iwe kuu. Moyo umetulia, amani umepata, wamwombao yeye.