164. Tumekujia Bwana Wetu
1. Tumekujia Bwana wetu
kujiweka mkononi mwako,
tuwe wako hata milele
twakushukuru na twakusifu.
Mwokozi wetu, utukubali,
utuongoze njia ya mbingu.
2. Twataka kubatizwa leo
kwa Jina lako, tuwe Wakristo.
Umetukomboa na sisi
ulipokufa pale Golgota,
na kwamba wewe upo karibu,
unasikia kuomba kwetu.
3. Twakupambia mioyo leo,
ingia, Mfalme wa utukufu!
Utupe sisi nuru yako
tuwe mwanga katika dunia.
Pokea leo mioyo yetu,
tunajitoa kwako wenyewe.
4. Tunakuomba sasa, Bwana,
usitutie majaribuni.
Utuongoze siku zote,
tukufuate wenye imani.
Mwisho tufike kwenye enzi kuu,
tuipokee taji ya mbingu.
Comments
Post a Comment