182. Nuru ya Rohoni
1. Nuru ya rohoni ni Bwana Yesu.
Nakuomba sana niangazishe;
ukanitazame kwa huruma tu,
/: Ukanitulize
mimi maskini. :/
2. Futa dhambi zangu
kwa damu yako.
Hasira ya Mungu iniondoke.
Machubuko yako, hata mateso,
/: Niyawaze vema
rohoni mwangu. :/
3. Nakutumaini peke yako tu,
niwe mtumwa wako
pote nilipo, utanikubali,
sina mashaka!
/: Nitakushukuru
pasipo mwisho. :/
Comments
Post a Comment