174. Ewe Baba, Bwana wangu

1. Ewe Baba, Bwana wangu,

   nielekeze mwenendo 

   nifuate Neno lako 

   hata leo kaa kwangu! 

   Uwe mlinzi na ngao

   uongoze maisha mpaka nifike

   kwako!


2. Umenipa na wazazi 

   walio mkono wako,

   wanifundisha vizuri, 

   hata na wadhamini, 

   walimu na wakuu 

   Baba Mungu naomba 

   nao uwaongoze!


3. Hata ndugu zangu wote 

   umenipa kwa wema, 

   nisaidiane nao 

   siku zote kwa pendo.

   Utupe kuungana

   wakubwa tuheshimu 

   kwa maneno mazuri!


4. Ulikuze kundi letu 

   tukae na adabu, 

   tuinue nchi yetu 

   siku zitungojazo!

   Nao ufalme wako 

   uenezwe na kwetu,

   uheshimiwe! Amen.

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima