213. Nakushukuru Mungu

1. Nakushukuru Mungu

   kwa kinywa na moyo 

   saa hii ya asubuhi 

   hata siku nzima. 

   Nitakuimbia, nitakusifu Baba,

   alivyonifundisha 

   Mwanao wa pekee. 


2. Umenilinda Bwana,

   usiku kucha huu 

   ukaondoa shida, 

   hatari na msiba. 

   Nakuomba sasa:  

   Uondoe makosa 

   niliyokukosea 

   kwa neno na tendo.


3. Nilinde hata leo 

   kwa neema yako tu,

   asinishinde mwovu 

   kwa hila yake kuu.

   Nisione shida 

   ya moto na ya maji, 

   ya homa na ugonjwa,

   ya kufa kubaya.

 

4. Mungu atanitunza 

   aliye Mwenyezi, 

   ayabariki yote nitakayotenda.

   Namwekea Yeye 

   uzima hata kufa,

   anitendee yale

   yanayompendeza. 

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima