167. Ni Siku Kuu Siku Ile
1. Ni sikukuu siku ile
ya kumkiri Mwokozi!
Moyo umejaa tele,
kunyamaza hauwezi.
Siku kuu! Siku kuu!
ya kuoshwa dhambi
zangu kuu.
Hukesha na
kuomba tu,
ananiongoza miguu.
Siku kuu! Siku kuu!
Ya kuoshwa dhambi
zangu kuu.
2. Tumekwisha kupatana
mimi wake, Yeye wangu,
na sasa nitamwandama,
nikiri Neno la Mungu.
Siku kuu! …
3. Moyo tulia kwa Bwana
kiini cha raha yako, huna njia
mbili tena:
Yesu ndiye njia yako.
Siku kuu! …
4. Nadhiri yangu ya mbele
nitaiweka daima,
hata ije siku ile
ya kuonana salama.
Siku kuu! …
Comments
Post a Comment