205. Ametwaliwa Rafiki Yetu

1. Ametwaliwa rafiki yetu 

   hatutamwona tena mwilini.

   Ameondolewa hapa petu,

   tunamzika mwili kaburini.


2. Ametwaliwa tuliyempenda,

   twajua ni mapenzi ya Mungu.

   Hayupo kwani Mungu amwita,

   aingie kundini pa Mungu.


3. Ametwaliwa kutoka kwetu, 

   lakini tutaonana tena.

   Yu katika furaha ya kweli, 

   na kule tutaimba pamoja!


Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima