186. Mfalme wa Upendo Ndiye
1. Mfalme wa upendo ndiye
anichungaye mimi,
Yeye ni wangu milele,
ananipenda daima.
2. Kwenye maji ya uzima
hunipeleka mimi
katika malisho mema,
anilisha siku zote.
3. Mara nyingi napotea
kwa ukaidi wangu,
naye ananitafuta,
na kunirudisha kwake.
4. Kivuli cha kufa kwangu
sitaogopa tena,
ukiwa kwangu daima
mashaka wayaondoa.
5. Wanitandikia meza,
naula mkate wako,
nanywa katika kikombe
nikumbuke kufa kwako.
6. Siku zangu zote hapa
wema wako u vivyo.
Nikubali Mchunga mwema,
nikuimbie milele.
Comments
Post a Comment