217. Ee Yesu Mesiya
1. Ee Yesu Mesiya,
Usiku umekwisha.
Mwanga wa huruma,
wanizunguka tena.
Vyote vimeamka,
vyakusifu wewe,
hata mimi Yesu,
ninakutukuza!
2. Ninaamka sasa
nazivaa nguo zangu,
hata roho yangu,
uipambe mwenyewe,
wongofu na pendo
na uvumilivu viwe pambo langu,
univike hivyo!
3. Uliye popote ukae hata kwangu,
nilinde kwa wema
katika njia zangu!
Nikusifu wewe
kwa mwenendo wangu,
kwa neno na tendo
siku zangu zote.
4. Nakuomba tena: Uzibariki vema
kazi zangu zote
ninazofanya leo!
Naye Roho wako
atawale kwangu,
niwe mtoto wako
hapa na huko juu.
Comments
Post a Comment