227. Kaa Nami ni Usiku Tena

1.  Kaa nami, ni usiku tena;

    Usiniache gizani, Bwana; 

    Msaada wako haukomi; 

    Nili peke yangu, kaa nami.


2.  Siku zetu hazikawi kwisha,

    Sioni la kunifurahisha; 

    Hakuna ambacho hakikomi,

    Usiye na mwisho, kaa nami.


3.  Nina haja nawe kila saa; 

    Sina mwingine wa kunifaa; 

    Mimi nitaongozwa na nani

    Ila Wewe? Bwana, kaa nami.


4.  Sichi neno uwapo karibu; 

    Nipatalo lote, si taabu;

    Kifo na kaburi haviumi; 

    Nitashinda kwako, kaa nami.


5.  Nilalapo nikuone wewe,

    Gizani mwote nimulikiwe;

    Nuru za mbinguni hazikomi, 

    Siku zangu zote kaa nami.


Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima