207. Lala Rafiki, Lala Mpenzi

1. Lala rafiki, lala mpenzi 

   laza kichwa chako kwa Mwokozi.

   Lala vyema, lala usingizi, 

        lala, lala vyema.


2. Aa! mpenzi sisi twakupenda,

   si kama akupendavyo Bwana.

   Mapenzi yake yazidi sana. 

        Lala, lala vyema.


3. Ulivyolala ni kama mwana 

   huamki kwa taabu tena. 

   Raha kule utulivu sana.

       Lala, lala vyema.


4. Hata jua tukufu litoke

   hata watu wema wafufuke.

   Waje na Yesu waume, wake. 

          Lala, lala vyema.


5. Siko kuagana, si ‘kwa heri’

   punde atakuja tumkiri. 

   Uwe mmoja kwake wa heri. 

         Lala, lala vyema.


6. Mpaka tuonane mbele zake, 

   na mavazi awapayo wake.

   Hata ya siri yafunuliwe. 

         Lala, lala vyema

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima