183. Usiku Ulipotolewa

1. Usiku ulipotolewa,

   Yesu, umetugawia 

   mapato ya mateso yako,

   tukumbuke kufa kwako.

   Waaminio wakusifu 

   wakija karamuni kwako.


2. Tunakumbuka kufa kwako,

   tukila  mwili wako huu; 

   twapewa nguvu ya uzima 

   tukinywa damu yako hii.

   Karamu hii tunayopewa 

   yatuonyesha pendo lako.


3. Huu mkate ni chakula kweli,

   hii damu yatutuliza;

   mioyo yetu yapumzishwa 

   tukila mezani kwako. 

   Tunaongezwa nguvu zetu, 

   za kukutegemea vema.


4. Twashirikiana na wote

   walio viungo vyako; 

   kwani tunashibishwa sote 

   kwa mwili na damu moja, 

   tu kundi la Mchungaji mmoja; 

   kwa hivi twapatana sote.


5. Twapewa mwili wako Bwana,

   tujue kweli ya kwamba 

   miili yetu ya unyonge 

   itageuka vizuri.

   Tutapokea mwisho kwako 

   miili mipya ya uzima.


6. Watupa mema mengi 

   Bwana Mwana Kondoo wake

   Mungu,

   mwenyewe u chakula chetu,

   kweli twatunzwa vizuri. 

   Twakila hapa kwa uchungu,

   lakini kwako kwa furaha.


Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima