209. Jua Likicha Linanyang’aza

1. Jua likicha linayang’aza

   mashamba yetu kwa 

   utukufu wa nuru yake

   yenye neema kuu.

   Nimelegea maungo usiku; 

   sasa ni macho, naona furaha

   nikitazama viumbe vyote.


2. Njooni tuimbe tukamtolee

   Muumba sadaka za mioyo yetu,

   mambo mazuri tuliyo nayo.

   Mungu ataka mioyo ya watu,

   nyimbo za sifa na za 

   kumshukuru,

   ndizo sadaka zimpendezazo.


3. Kazi ya Mungu ni kila siku 

   kutubariki, kutuongoza,

   kutukingia hatari nyingi,

   sisi twalala, Bwana anakesha;

   tukiondoka, anatung’azia

   mwanga mzuri wa huruma yake.


4. Mambo ya watu, yote yapita.

   Mambo ya Mungu yanasimama.

   Neno la Bwana lakaa milele.

   Atutolea wokovu wa neema,

   ayaondoa machungu ya kufa,

   tuwe wazima hapa na huko.


5. Mwenye huruma unisamehe

   makosa yangu, uyaondoe 

   machoni pako kwa neema yako.

   Tena naomba: Nilinde vizuri,

   uniongoze na kunitawala 

   kama mwenyewe 

   unavyopenda.


6. Msiba na shida mwisho zapita;

   kama twaona mwanga wa jua

   baada ya mvua mbinguni tena.

   Raha, uzima, furaha, amani

   zaningojea mbinguni kwa 

   Mungu:

   Ninatamani furaha za juu.


Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima