154. Ninataka Kuingia
1. Ninataka kuingia
mjini kwa Mungu.
Nitashinda, nitakaza
mwendo nifike,
nikishikwa na shida,
nikichoka njiani,
Yesu unaniambia:
“Uningojee!”
2. Naitwa na Yesu Kristo
enzini mwake.
Nakimbia, kukawia
hakuna faida,
wote wachelewao
hawatapata taji.
Mimi sitaki kingine
ila uzima.
3. Elekeza macho yangu
mlangoni pako.
Niongoze, nipe nguvu,
ninapochoka.
Ninapojaribiwa,
ninaposingiziwa,
Yesu, unisaidie
nisikuache.
4. Mkono wako
unishike nisianguke.
Najiona kuwa mnyonge,
nguvu i kwako,
Neno lako, ee Yesu,
linanipa uzima.
Nikifika, nitaimba,
“Umeniponya!”
Comments
Post a Comment