188. Sioshwi Dhambi Zangu
1. Sioshwi dhambi zangu,
bila damu yake Yesu.
Hapendezewi Mungu,
bila damu yake Yesu.
Hakuna kabisa
dawa ya makosa
ya kututakasa,
ila damu yake Yesu.
2. La kunisafi sina,
ila damu yake Yesu.
Wala udhuru tena,
ila damu yake Yesu.
Hakuna kabisa …
3. Sipati patanishwa,
bila damu yake Yesu.
Hukumu yanitisha,
bila damu yake Yesu.
Hakuna kabisa …
4. Sipati tumaini,
bila damu yake Yesu.
Wema wala amani,
bila damu yake Yesu.
Hakuna kabisa …
5. Yashinda ulimwengu,
hiyo damu yake Yesu.
Na kutufikisha juu,
hiyo damu yake Yesu.
Hakuna kabisa …
6. Twaimba, “Utukufu
una damu yake Yesu”.
Milele twaisifu
hiyo damu yake Yesu.
Hakuna kabisa …
Comments
Post a Comment