150. Ahimidiwe Mwamba Wangu
1. Ahimidiwe mwamba wangu,
ahimidiwe ngome yangu, wema
wake wapita vyote duniani.
2. Aturuzuku kila kitu,
atugawia mema kwetu
wema wake wapita vyote
duniani.
3. Upendo wake mwingi sana,
katutolea Mwana wake, wema
wake wapita vyote duniani.
4. Katika Yesu, Mwana wake,
Twapatanishwa naye Baba,
wema wake wapita vyote
duniani.
5. Ashukuriwe Mungu wetu,
sifa zote ni zake Bwana
wema wake wapita vyote
duniani.
Comments
Post a Comment