179. Yesu Kwa Imani

1. Yesu kwa imani, nakutumaini, 

   peke yako. 

   Nisikie sasa na kunitakasa,

   ni wako kabisa tangu leo.


2. Nipe nguvu pia za kusaidia

   moyo wangu.

   Ulikufa Wewe, wokovu nipewe,

   nakupenda Wewe, 

   Bwana wangu.


3. Hapa nazunguka 

   katika mashaka, na matata. 

   Palipo na giza utaniongoza 

   hivi nitaweza kufuata.


4. Takuwa mzima

   nivushe salama mautini. 

   Sina hofu kamwe 

   ukiwapo nami, 

   nami nikwandame siku zote.

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima