176. Tumiminie ee Mtakatifu
1. Tumiminie ee Mtakatifu,
Roho wako mwenye nguvu
atakase mioyo yetu,
tuwe wako tu kale na kale!
2. Wewe mwenyewe,
tulinganishe
tuungame kwa furaha,
ya kuwa u Bwana wetu,
tena Mwokozi
kwa damu yako!
3. Tukutazame
kwa mioyo yote,
tukilirudisha upya
agano la ubatizo,
tukufuate, tuache yetu!
4. Tukija sasa kubarikiwa,
sikia kuomba kwetu,
tugawie mema mengi,
tutengemane
mwangani mwako!
5. Na atujie Roho wa Bwana,
atuunganishe sote
kuwa kundi takatifu
mpaka tumwone
kwake mbinguni!
Comments
Post a Comment