228. Jua Limekuchwa
1. Jua limekuchwa, waja usiku,
twakaa na Yesu rohoni mwetu.
2. Nyota zatokea, ndege watua,
kazi imekwisha, mwili walala.
3. Bwana ukumbuke wakuitao,
ukawatulize na waumwao.
4. Ndoto za watoto zitoke kwako,
tukifumba macho, utubariki!
5. Wasafiri bara na baharini,
linda, wazuie na wakosaji!
6. Hata asubuhi tunapoamka,
upendezwe nasi, tukikushika.
Comments
Post a Comment