202. Watu wote Yawapasa

1.  Watu wote yawapasa 

    kufa kama majani.

    Wakaao duniani, 

    yawapasa kuzikwa, 

    na kuoza kaburini, 

    wakitaka kugeuka 

    na kuona furaha, 

    tuliyoahidiwa.


2.  Hata mimi ni tayari, 

    nitamwekea Mungu 

    roho yangu akitaka,

    kuniita kufani. 

    Kwani nimekombolewa

    na Mwokozi wangu Yesu,

    kufa kwake kuchungu 

    kumenipa tulizo.


3. Yesu amenikomboa

   akinifia mimi.

   Sasa mimi nitaacha 

   kwa furaha dunia,

   na kuingia mbinguni 

   kwake Mungu Mwenye enzi,

   na kwa Yesu Mwokozi 

   katika furaha kuu.


4. Kule wateule wengi 

   wanapomtumikia Mungu

   penye kiti chake,

   ni mahali pazuri.

   Na malaika waimbapo

   nyimbo za kumsifu Bwana:

   Ee Mungu Mtakatifu,

   Baba, Mwana na Roho.


5. Waliko wazee wa kale,

   wafumbuaji wa Mungu; 

   kule wanakaa mitume 

   juu ya viti vya enzi;

   kule wamekusanyika 

   waliotutangulia,

   kule tutasikia

   Haleluya daima.


6. Naona Yerusalemu 

   unang’aa kwa mwanga mkuu 

   Nasikia sauti nzuri

   za vinubi na nyimbo.

   Kweli ni furaha kubwa, 

   kule jua litokapo 

   unapopambazuka

   mchana usioisha.


7. Nimeona haya yote

   rohoni kwa furaha.

   Basi ninapenda kwenda

   kuingia mbinguni! 

   Ndugu zangu: Kwaherini! 

   Mungu awalinde nyote.

   Kwaherini! Nakwenda, 

   imekwisha safari


Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima