168. Shika Mikono Yangu
1. Shika mikono yangu, niongoze,
mpaka nimalizapo safari hii.
Nikiwa peke yangu napotea.
Popote uendapo nipeleke!
2. Tuliza moyo wangu, uwe kimya,
nikiona furaha au majonzi,
unitulize sana, ndimi wako,
sitaki neno tena, ila hilo.
3. Nisipoona leo nguvu yako,
najua wanilinda, huniachi.
Shika mikono yangu niongoze,
mpaka nimalizapo safari hii!
Comments
Post a Comment