224. Kukichwa Watu Wote

1. Kukichwa watu wote

   na wanyama nyumbani 

   na ndege walala.

   Ee moyo wangu sasa 

   uanze kufikiri 

   ninavyompendeza Mungu.


2. Jua limeingia, Giza limetokea, 

   usiku karibu. 

   Jua lingine sasa 

   lang’aza moyo wangu:

   Ni Yesu, Mwokozi wangu.


3. Miguu hata mikono 

   inafurahi sana, kazi imekwisha.

   Nao moyo wataka 

   kukombolewa hivyo

   katika nguvu za mwovu.


4. Nafumba macho yangu, 

   nalala usingizi, sijui lolote.

   Wewe uangalie

   roho na mwili wangu,

   uliye mlinzi wetu mkuu.


5. Yesu furaha yangu, 

   unifunike sasa, unikumbatie.

   Uagize malaika 

   wanikingie shida,

   Shetani akinitaka.


6. Hata wapenzi wangu 

   nawaombea wote 

   wasione shida. 

   Mungu atawalinda 

   kwa jeshi la malaika 

   walale wote kwa raha.


Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima