149. Chini ya Bawa Lako
1. Chini ya bawa lako,
ee Yesu nifiche
Unipe raha kwako
kwenye mambo yote.
Na uwe yote kwangu,
hekima, shauri,
na siku zangu zote
niwe na amani.
2. Nisamehe makosa
nioshe kwa damu,
unipe nia safi
na mapenzi mapya.
Wakubwa na wadogo
ututunze sote,
na kwa amani yako
tupate furaha.
Comments
Post a Comment