196. Upendo wa Mungu Wetu
1. Upendo wa Mungu wetu
ndio jua letu.
Hutung’azia moyoni
hufuta uchungu.
Giza hukoma na mchana
hutokea sasa,
furaha tupu na shangwe
huwamo moyoni.
Upendo huu una nguvu
tangu mwanzo na daima,
atupenda mimi nawe,
tuwe karibu na Yeye.
2. Tangu mwanzo Baba Mungu
alivyotuumba,
ametuonyesha pendo
kwa kutukumbuka.
Hutupa mema mengi mno
duniani petu,
ila sisi hatukumpa
shukrani ya kweli.
Upendo huu …
3. Ndipo akamtuma Yesu
mwenye pendo jingi.
Awaza, “Pendo la kufa,
watalikubali?”
Atuamsha atuita,
“Acheni mabaya!”
Tumjue anavyopenda
kutupa uzima.
Upendo huu …
4. Nasi tudumu pendoni
Yesu Bwana wetu
Yeye jua la baraka
mioyoni mwetu.
Tumwamini na tumpende
sasa na milele.
Amani tupu, rehema
zatoka kwa Yesu.
Upendo huu...
Comments
Post a Comment