184. Moyo Wangu Ujipambe

1.  Moyo wangu ujipambe,

    acha mambo ya gizani. 

    Kaza mwendo wa nuruni 

    hivi utang’aa vizuri. 

    Kwani Bwana wa rehema 

    akukaribisha kwake. 

    Mwenye utukufu mwingi

    anapenda kuja kwako.


2.  Amka ukamlaki yeye, 

    umkaribishe vizuri.

    Abishaye hodi kwako, 

    akuleteaye neema.

    Umkubali kwa furaha 

    aingiaye moyoni.

    Sema: Bwana, nakupenda, 

    sikuachi siku zote.


3.  Hatuwezi kufahamu 

    mambo haya ya ajabu:

    Unapenda kuwa nasi 

    kwa mkate na kwa mvinyo.

    Yesu, tunaomba sana: 

    Wewe kaa leo hapa, 

    tugawie neema yako, 

    Chakula Kitakatifu.


4.  Yesu, jua la rehema,

    Yesu,chemchem ya uzima,

    Yesu, nakupenda sana,

    nuru ya maisha yangu. 

    Nakuomba: nibariki 

    nikila chakula chako 

    nipe nguvu ya uzima, 

    tuishi wewe na mimi.


5.  Pendo limekuhimiza 

    kutafuta wakosaji. 

    Umetoa mwili wako 

    kutulisha roho zetu, 

    ukamwaga damu pia 

    ili utunyweshe sisi.

    Twakumbuka pendo hili 

    hapa karamuni kwako.


6.  Yesu, mkate wa uzima, 

    nijalie nisikose 

    msaada wa karamu yako,

    nisijiponze nikila. 

    Nikumbuke, mambo haya 

    yaonyesha pendo lako. 

    Unisaidie, niwe 

    mgeni wako kwa milele.


Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima