193. Ndoa Yetu Nzima

1.  Ndoa yetu nzima simika, Yesu!

    Usiku na mchana uwepo kwetu.

    Leo tuna raha, Wewe watupa.

        /: Ndoa yetu Bwana  

         ndiwe baraka!/:


2.  Atoka kijana, ataka mchumba

    siku zinapita  za kupimana.

    Leo twapatana pamoja kukaa 

        /: Ndoa yetu … /:


3.  Vyote hapa chini vinakaa muda,

    vyote vinaoza, tena vyachakaa. 

    Pendo la dunia nalo huchakaa. 

         /: Ndoa yetu … /: 


4.  Kaa kwetu Bwana, kutukagua,

    pendo letu sisi lisichakae: 

    Hivi natukae na baraka tu. 

          /: Ndoa yetu … /:


5.  Kana arusini ulialikwa, 

    walivyoishiwa ukaongeza, 

    nasi shida zetu utazishinda. 

          /: Ndoa yetu … /:

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima