201. Mwenzetu Kazi Yako Imekwisha
1. Mwenzetu kazi yako
imekwisha duniani.
Umekwisha kutua
mzigo wa shida na taabu.
Yesu tupe kufika
walipo washindaji.
2. Yesu ni kiongozi
katika bonde la kufa.
Amekutangulia
kaburini na peponi.
Yesu tupe …
3. Wewe wachukuliwa
na malaika kwa Mwokozi.
Utapokewa sasa
na wateule wa Mungu.
Yesu tupe …
4. Mwili wako wazikwa,
ugeuke kuwa vumbi.
Twatumaini kwamba
ufufuko utakuwa.
Yesu tupe …
5. Sasa unapandwa tu
kama mbegu ya shambani.
Mpaka yaje mavuno
siku ya kufufuliwa.
Yesu tupe …
Comments
Post a Comment