194. Yesu Nitakuimbia
1. Yesu nitakuimbia
kwa rehema zako zote.
Baraka nyingi sana
nimepata kwako Bwana.
Wewe ulinikomboa
kwa maumivu yako.
2. Yesu nitakuimbia
hapa siku zangu zote.
Nitakapokumbuka,
neema na huruma zako.
Yesu nitakuimbia,
sababu wanilinda.
3. Yesu nitakuimbia
katika maisha yangu.
Napenda kuingia
Bwana wangu unapokaa,
nikuimbie na malaika
milele na milele.
Comments
Post a Comment