152. Mahali pa Raha
1. Mahali pa raha ya moyo wapi?
Akukingiaye mabaya nani?
Dunia haina makimbilio,
nisiposhindwa na makosa yangu.
/:Sipo, sipo hapa sipo,
mbinguni ni ngome
ya moyo wangu. :/
2. Iache dunia, uone ngome,
unapofurahishwa moyo wangu.
Ni Yerusalemu unaojengwa
na mawe mazuri ya dhahabu tu.
/: Ndiko, ndiko,
ndiko ngome
na makimbilio
ya moyo wangu. :/
3. Mwangani kwa Yesu
ni raha tamu,
hakuna makosa na shida huko.
Vinubi na sauti za nyimbo nzuri
zinaufurahisha moyo huko.
/: Raha, raha, raha tamu
mbinguni kwa Yesu
naitamani. :/
Comments
Post a Comment