204. Wenye Mizigo Njooni
1. Wenye mizigo njooni,
nitawapumzisha.
Tusikilize sauti,
sauti yake Bwana.
Inatupa habari
ya baraka nyingi
dhambi huondolewa,
furaha inakaa.
2. Enyi wanyonge njooni,
nitawapa nguvu.
Wote sikilizeni
mbali na karibu!
Adui zetu wengi,
watupinga sana,
kwa nguvu ya Mwokozi
wote watashindwa.
3. Kila ajaye kwangu,
simfukuzi kamwe.
Sauti ya pendo hili
yatufurahisha.
Yesu aita wote
walio na dhambi,
wamjie wakapate
raha na mapenzi.
Comments
Post a Comment