158. Liko Pumziko la Mioyo
1. Liko pumziko la mioyo,
amka wee unayechoka,
Unaugua kama mfungwa kwa
shida za moyo wako
Umtazame Kondoo wa Mungu
atakuchunga kwa furaha.
Uache mzigo enenda.
Vita nzuri yamalizika,
safari yabaki kidogo
inayokusumbua mno.
2. Mungu ametuchagulia
pumziko lisilo mwisho
Amelitengeneza kale,
mtu hajazaliwa bado,
kufa kwamfurahisha Mponya,
tupate pa kupumzikia.
Aita, anaalika
mioyo inayokaa na shida,
msikawie, njooni leo!
Ingieni pumzikoni!
3. Ninyi mshindwao na mizigo
mlemewao na uzito
Rukeni kimbieni hima,
tokeni pangoni mwenu;
msienende kwa kuinama,
Mponya anawaambieni:
Mimi ni pumziko lenu,
ninyi wana wote wa Mungu.
Popote mwalizwa na shida,
kwa Yesu mwanyamaa kimya!
4. Hapo pumzikeni rahani,
wasiwasi hatunao.
Shikeni Neno hili jema:
Pumzikeni, Yesu yuko!
Shikeni mabawa upesi,
karukieni kama ndege
Wako jamaa wanangoja;
Furahi moyo, shangilia,
patana nao utukuze,
uko mwaka wa pumziko!
Comments
Post a Comment