163. Mungu Upokee Moyo Wangu

1. Mungu upokee 

   moyo wangu wote,

   niwe mtoto wako, 

   siku zangu zote.

   Nikufuate Wewe 

   nisikuache tena, 

   nishike siku zote, 

   ulivyotuagiza.

   Unisaidie mimi, 

   hata kufa kwangu.


2. Msalabani pako, 

   Yesu naanguka, 

   uliyenifia

   hata mimi pia.

   Yaondoe makosa 

   yatoweke kabisa, 

   nipate kuwa safi 

   kwa damu yako bora.

   Unisaidie mimi 

   hata kufa kwangu.


3. Roho Mtakatifu, 

   unanipa nguvu;

   niweze kushinda 

   majaribu yote, 

   naomba: utawale 

   katika moyo wangu,

   Shetani, hata kufa, 

   asinishinde mimi.

   Unisaidie mimi,

   hata kufa kwangu.


4. Baba, Mwana, Roho 

   uliye mmoja tu, 

   niliye  maskini

   nakuomba sana: 

   Unikubali sasa,

   katika ubatizo, 

   futa makosa yangu 

   kwa maji haya bora.

   Unisaidie mimi,

   hata kufa kwangu.

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima