206. Kuna Nchi Nzuri Mbali Sana
1. Kuna nchi nzuri mbali sana.
Wako watu wema, wasimama,
waimba vizuri sifa zake
Mwokozi,
nasi duniani twamtukuza.
2. Njooni kwa nchi hii njooni sasa!
Mbona mwasimama
mashakani?
Tuache makosa,
yanamchukiza Bwana.
Kwake tutaketi kwa salama.
3. Machozi hapana,
wala hamu,
mbele yake Baba
mapenzi tu.
Utaona raha utapewa
kilemba kuvikwa na wale wa
mbinguni!
Comments
Post a Comment