185. Bwana Wetu Ametoa
1. Bwana wetu ametoa
mara moja msalabani
mwili na maisha yake
kwa wokovu mkamilifu.
2. Ndiye kafara ya kweli
itoshayo siku zote;
kima chake ni kikubwa
hakiwezi kuzidishwa.
3. Mbinguni atuombea
akiwa kitini pake.
Na hapa atubariki,
tukila karamu yake.
4. Twaonyesha kufa kwake
mpaka atakaporudi;
tunaungana na Yeye
kuwa viungo vyake tu.
Comments
Post a Comment