197. Ukimpata Mwenye Moyo
1. Ukimpata mwenye moyo
mwaminifu daima,
umepata kito bora,
wajaliwa na Mungu.
Japo nimo shidani,
hali yangu ya heri.
2. Ukiingiwa na taabu
na kupatwa na msiba,
mwenzi wako mwaminifu
atakutia moyo.
Japo nimo shidani
3. Haja yake mwenzi huyu
kukusaidia tu.
Taabu yako ndiyo yake,
hakuachi msibani.
Japo nimo shidani...
4. Rafiki wa duniani,
mali zitapotea,
mwenzi wako mwaminifu
atakaa kwa mpenziwe.
Japo nimo shidani …
5. Mtu kuwa na mwenzake
mwaminifu daima,
ndiyo hali duniani
ipitayo kabisa.
Japo nimo shidani...
Comments
Post a Comment