208. Ee Moyo Wangu Amka
1. Ee moyo wangu amka,
mwimbie Mwumba wako,
aliyetupa neema,
atulindaye sote.
2. Nilipolala leo,
usiku wewe Baba
umenilinda vema,
sikuwa na hatari.
3. Wasema: “Mtoto wangu,
usiogope kitu,
ulale usingizi,
nitakuamsha kesho”
4. Nimevipata vile
ulivyoniambia.
Naona mchana tena
na nguvu na uzima.
5. Nilipe jinsi gani
ulivyonitendea?
Nakupa moyo wangu
sina kizuri zaidi.
6. Huwezi kukataa
kipaji kama hicho.
Wajua kama sina
mengine ya kukupa.
7. Maliza kazi yako
uliyoanza kwangu,
tuma malaika wako
anikingie msiba.
8. Kubali nitendayo,
unipe shauri jema,
kuanza na kuisha
ni shauri lako, Bwana.
9. Unibariki leo,
nishike njia yako.
Nenolo la uzima
liniongoze kwako.
Comments
Post a Comment