203. Yesu Bwanangu Shujaa

1. Yesu Bwanangu shujaa 

   na Mwokozi anaishi. 

   Nikijua haya tu,

   ninaweza kutuliza moyo wangu 

   ukiwa wenye woga wa kufa.


2. Yesu Mwokozi wangu,

   Anaishi hata mimi 

   nitaishi mahali, 

   atakapokaa Bwanangu, 

   kwani viungo hukaa 

   palipo kichwa chao.


3. Nimeungana naye, 

   nikimtumaini yeye.

   Ninamshika kwa nguvu, 

   nikimtegemea kweli. 

   Hata nguvu ya mauti 

   hainitengi naye.


4. Mwili wangu wa sasa

   utaoza kuwa vumbi.

   Baadaye na Yeye 

   atanifufua tena,

   niwe mbinguni kwake 

   na kumwona milele.


5. Wenye unyonge hapa, 

   kule watapata nguvu.

   Napandwa kwa aibu, 

   kule nina utukufu.

   Ninapandwa kwa mwili, 

   nitaishi kwa roho.


6. Furahini viungo 

   vya Mwokozi hampotei 

   iacheni huzuni,

   Yesu atawafuata, 

   ikilia panda kuu 

   iwaamshayo wafu. 

 

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima