1. Mwezi umechipuka na nyota zamulika mbinguni popote. Makonde yote kimya, na kunako mabonde ukungu mzuri unakaa. 2. Dunia imekuwa nchi ya utulivu, ni nyumba ya raha. Viumbe vyenye taabu, waume, wake, wana na watulie usiku. 3. Tukiwa na kiburi, tu wakosaji sana, wapuuzi kabisa. Twatunga vya uongo, na maarifa yote yametutenga na Mungu. 4. Utuonyeshe, Mungu, wokovu wa kikweli, tusijidanganye! Tukae duniani kama watoto wema wamtegemeao Baba. 5. Na sasa ndugu zangu, tuende kujilaza kwa Jina la Mungu. Atupe usingizi sisi tuliochoka, hata majirani wote!
1. Ee moyo wangu, hima, enenda mbinguni! Ulimwenguni humu hapana pa raha. Mchungaji wetu Yesu achungapo kondoo ni penye raha kuu. Enenda mbinguni! 2. Yeye akupokee, Mungu Baba yako, akuketishe pake katika enzi kuu. Atakuvika nguo za wongofu wa Mungu, akupa raha kuu. Enenda mbinguni! 3. Nakutamani sana Mwana Kondoo Mungu! Ningepata mabawa ningeruka pale, wanaposhangilia malaika wake Mungu katika raha kuu. Enenda mbinguni! 4. Mapenzi yako Bwana ndizo haja zangu, Utakalo lolote nami nitatenda. Naingojea siku utakayoniita, nipate raha kuu!...
Mwenyezi, Mwenyezi, Mwenyezi, Jina lako litukuzwe sana. Amin, Amin. Hata ulimwengu wetu uteketezwe kwa moto. Nazo nyumba zetu, ziimbe utakatifu wake, Haleluya, Haleluya.
Comments
Post a Comment