200. Sijui Saa ya Kufa Kwangu
1. Sijui saa ya kufa kwangu,
maisha yangu yapita.
Naomba Mungu, Bwana wangu
kwa ajili ya Mwanao.
Shika roho yangu,
kwa furaha,
niache ulimwengu huu.
2. Tukiwa hapa duniani
kufa kunatuvizia,
hakutuwekei kiaga,
kunakuja kwa haraka.
Shika roho …
3. Unifundishe nifikiri,
vizuri mambo ya kufa.
Nijutie makosa yangu,
yaondolewe na Yesu.
Shika roho …
4. Unipe nguvu, nijiweke
tayari kwa mambo yote.
Niweze kuitika vema,
ukiniita kwa kufa.
Shika roho …
5. Baba, ondoa dhambi zangu
kwa damu ya Bwana Yesu.
Najificha katika huyu,
kwani amenikomboa.
Shika roho ...
6. Nikiwa naye Bwana Yesu,
sioni hofu ya kufa.
Na saa ya kufa ikifika,
namtumaini Yesu tu.
Ninajua kwa damu ya Yesu
napata kufa kuzuri.
Comments
Post a Comment