211. Muumbaji wa Vitu Vyote

1.  Muumbaji wa vitu vyote 

    Baba, Mwana na Roho, 

    uletaye kila siku,

    jua, mwezi, na nyota, 

    ulindaye vizuri  

    viumbe vyako vyote.


2.  Ninakushukuru Baba,

    kwamba umenilinda, 

    ukanikingia tena 

    shida, woga, huzuni,

    hata hila ya mwovu 

    haikunipoteza. 


3.  Niongoze Bwana wangu, 

    kwa nenolo siku hii.

    Uwe mlinzi wangu leo,

    nisikose kukutii.

    Usiponiongoza 

    sina budi kukosa.


4.  Umtume malaika wako 

    anishike vizuri, 

    akazizuie hila,

    majaribu na tamaa.

    Naye anichukue

    mwisho kwako mbinguni.


Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima