216. Babangu Kule Mbinguni
1. Babangu kule mbinguni,
aliye juu pa malaika,
/: aangalia njia zangu
na kunilinda maisha. :/
2. Hata unywele kichwani
hauanguki ovyo tu
/: na siri zote za moyoni
zajulikana kwa Baba. :/
3. Zamani nisipojua,
amekwisha kuandika
/: mkononi mwake jina langu,
ndio upendo wake mkuu.:/
4. Ee Baba yangu u mwema,
nami nataka kufanya
/: kama malaika wafanyavyo
mbinguni kwako milele!:/
Comments
Post a Comment