172. Nitwae Hivi Nilivyo

1. Nitwae hivi nilivyo, 

   umemwaga damu yako, 

   nawe ulivyoniita, 

        Bwana Yesu, naja, naja.


2. Hivi nilivyo si langu

   kujiosha roho yangu.

   Nisamehe dhambi zangu,

         Bwana Yesu, naja, naja.


3. Hivi nilivyo sioni 

   kamwe furaha moyoni.

   Daima ni mashakani, 

         Bwana Yesu, naja, naja.


4. Hivi nilivyo kipofu, 

   maskini na mpungufu. 

   Wewe u mtimilifu; 

        Bwana Yesu, naja, naja.


5. Nawe hivi utanitwaa, 

   nisithubutu kukawa, 

   na wewe hutanikataa.

          Bwana Yesu, naja, naja.


6. Hivi nilivyo mapenzi yamenipa

   njia wazi, hali na mali sisazi, 

          Bwana Yesu, naja, naja.

 

Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima