147. Mtakatifu Wewe, Mungu

1. Mtakatifu Wewe,

   Mungu Mwenye enzi, 

   jua likitoka tutakutukuza wee.

   Mtakatifu Wewe 

   wa huruma nyingi,

   Mwenyezi Mungu wa Utatu.


2. Mtakatifu Wewe, 

   waliookoka wakusujudia Wewe 

   huko daima.

   Makerubi wote wakuinamia,

   Mwenyezi Mungu wa Utatu.


3. Mtakatifu Wewe, siri wajificha, 

   macho yetu 

   hayawezi kukutazama, 

   Wewe peke yako 

   Mtakatifu kweli, 

   Mwenyezi Mungu wa Utatu.


4. Mtakatifu Wewe

   Mungu Mwenye enzi, 

   kazi zako zakusifu kila mahali. 

   Mtakatifu Wewe 

   wa huruma nyingi, 

   Mwenyezi Mungu wa Utatu.

   Amen. 


Comments

Popular posts from this blog

230. Mwezi Umechipuka

151. Ee Moyo Wangu, Hima