222. Bwana, Imepita Tena
1. Bwana, imepita tena
siku moja ya neema.
Nifundishe nifikiri
mambo yote ya leo.
Unionyeshe sasa
niliyokukosea.
Nimalize mambo yote
kad’ri ya mapenzi yako.
2. Kweli utaona mengi
yasiyokupendeza.
Kwani ni mtu wa makosa,
yaliyo mengi sana.
Moyo wangu, na kinywa,
na mikono yakosa
kwa kuwaza na kusema
na kutenda kila siku.
3. Nakuomba ewe Mungu
nihurumie tena.
Ondoa maovu yote
niliyokutendea.
Uyafute makosa
kwa rehema yako kuu.
Nitaangalia kesho
nizishike amri zako.
4. Bwana wewe unakesha,
sisi tukisinzia.
Macho yako hayachoki,
ndiwe Mchungaji mwema,
awalindaye kondoo
katika giza lote.
Utulinde sisi sote,
kondoo wako tulalapo.
5. Kukipambazuka tena
niondoke kwa bidii
nikutumikie vema
katika mambo yote;
utakaponiita nife leo usiku,
ninakuwekea Bwana,
roho mikononi mwako.
Comments
Post a Comment