226. Nimechoka Kabisa
1. Nimechoka kabisa
macho yangu mazito;
macho yako Babangu,
yanilinde usiku.
2. Niliyokukosea,
Mungu niondolee!
Damu ya Yesu Kristo
huning’aza kabisa
3. Ndugu zangu, ee Mungu,
uwalinde usiku;
wakubwa na wadogo
wote walale raha.
4. Wenye shida tuliza,
uwafute machozi,
uwapokee wote
wafao usiku huu.
Comments
Post a Comment