210. Kila siku Asubuhi
1. Kila siku asubuhi
Yesu anabisha hodi
mlangoni kwa wamwombao:
Bwana Yesu, njoo kwetu!
2. Tumfungulie milango
ya mioyo aingie,
Tumwalike kwa furaha:
“Bwana Yesu, njoo kwetu”.
3. Kaa kwetu siku zote,
ufukuze maadui,
wasiweze kutudhuru
sisi tulio wako.
4. Uwe Mchunga wetu mwema,
utulishe malishoni,
tukutumaini wewe
leo na siku zote.
5. Kweli Yesu atulisha,
anatuongoza leo.
Ni furaha yetu kubwa.
Tunakwenda na Yesu.
Comments
Post a Comment