153. Ninapenda Kwenda Zangu
1. Ninapenda kwenda zangu
nimwone Mwokozi
wangu.
Moyo wangu watamani
kuambatana na Yesu
/: na kumsifu milele. :/
2. Ninapenda kusikia
nyimbo za malaika wote.
Ningekuwa na mabawa
ningeruka leo hivi
/: mpaka Sayuni
kwake.:/
3. Ninapenda kuingia
pale penye utukufu,
penye nyumba za dhahabu
nimwone Mwokozi
wangu
/: na furaha za mbingu:/
4. Ninapenda kuuona
uzuri wa Paradiso.
Nikifika nitapata
tunda lake tamu sana,
/: Yesu, nipeleke juu! :/
Comments
Post a Comment