162. Bwana, Twakuletea
1. Bwana, twakuletea
mtoto huyu, (watu hawa)
tukijua amri yako ya mwisho
uliyowapa mitume:
Watu wote wabatizwe,
watakaokuwa wako.
2. Neno hili ni kubwa
tulilopewa na Yesu:
Atakaye kufika katika ufalme
wako,
hana budi kuzaliwa
tena kwa maji na Roho.
3. Pokea kondoo wako
Mchunga mwema Bwana Yesu
Umwongoze mbinguni
(Waongoze mbinguni)
ndiwe njia na uzima.
Umpe kukutegemea
(wape kukutegemea)
apate kutengemana
(wapate kutengemana).
4. Baba, tunakusihi
ukubali wimbo wetu,
usikie maombi
tunayokuomba sasa.
Andika jina la mtoto
(Andika majina yao)
katika kitabu chako!
Comments
Post a Comment