151. Ee Moyo Wangu, Hima
1. Ee moyo wangu, hima,
enenda mbinguni!
Ulimwenguni humu
hapana pa raha.
Mchungaji wetu Yesu
achungapo kondoo
ni penye raha kuu.
Enenda mbinguni!
2. Yeye akupokee,
Mungu Baba yako,
akuketishe pake
katika enzi kuu.
Atakuvika nguo
za wongofu wa Mungu,
akupa raha kuu.
Enenda mbinguni!
3. Nakutamani sana
Mwana Kondoo Mungu!
Ningepata mabawa
ningeruka pale,
wanaposhangilia
malaika wake Mungu
katika raha kuu.
Enenda mbinguni!
4. Mapenzi yako Bwana
ndizo haja zangu,
Utakalo lolote
nami nitatenda.
Naingojea siku
utakayoniita,
nipate raha kuu!
Enenda mbinguni!
Comments
Post a Comment