215. Tumsifu Bwana Sote
1. Tumsifu Bwana sote tumpendao
tumshangilie kwa furaha kubwa
na kumtolea sifa na shukrani.
Tumsifu Bwana!
2. Aliyelinda nguvu na uzima
aliyetupa Yeye leo tena.
Ametuamsha wenye hali njema.
Tumsifu Bwana!
3. Tukitumia nguvu za maungo,
tukisikia na kusema sawa
ndio baraka na huruma yake.
Tumsifu Bwana!
4. Mchungaji mwema,
atupaye yote,
twaomba: Utulinde hata leo,
tuone wingi wa rehema yako.
Tumsifu Bwana!
5. Tusaidie, tufuate leo
kwa nguvu zako
njia za kunyooka,
tusikuache na rehema yako.
Tumsifu Bwana!
6. Utufundishe kusikia Neno
na kulishika
kwa mwenendo mzuri.
Tusaidie tulio wanyonge.
Tumsifu Bwana!
7. Utuongoze, tusikose njia
tuwe watawa hapa duniani,
tukikumbuka siku ya hukumu.
Tumsifu Bwana!
8. Siku ya mwisho utakuja Bwana,
na kuongoza wateule wako
pale malaika wote waimbapo.
Tumsifu Bwana!
Comments
Post a Comment